MAOMBI YA KUSIMAMIA NENO
Kutana na mtu wa Mungu Nabii Samson analo neno la kinabii juu ya maisha yako
Utangulizi
Wengi wetu tunapenda Sana kufanya maombi, Maombi nijambo la muhimu sana kuomba kwakuwa Yesu akasema Ombeni bila kukoma maombi siyo swala la kuomba leo na kuache ni jambo endelevu la wakati wote Hapa Mungu amekupa neema ya kujifunza kanuni rahisi ya kuomba
Yeremia 1:12 Ndipo Bwana akaniambia, Umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu, ili nilitimize
Lile unaloliomba ni kwasababu umeliona au unaliona katika ulimwengu wa Ki Roho sasa likiwa linahusiana na Neno La Mungu lazima utalipata maombi tofauti na Neno la Mungu Hakuna majibu, haijalishi unaomba masaa mangapi au kwa muda gani omba kwa kusimamia Neno la Mungu na wewe utajibiwa,
Tumeruhusiwa kuomba lolote tutakalo
Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; Mathayo 7:7
Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. - Yohana 15:7
Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua. - Yeremia 33:3
Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. - Yeremia 29:13
Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia. - Isaya 65:24
Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao. - Mathayo 18:19,20
Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba. - I Yohana 5:14,15
ombeni bila kukoma; I Wathesalonike 5:17
Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia. Hakika Mungu amesikia; Ameisikiliza sauti ya maombi yangu. - Zaburi 66:18,19
Akasema, Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano; lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako. - Luka 22:31,32
Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee. - Waebrania 7:25
Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano. I Timotheo 2:8
Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu. - Warumi 8:26,27
Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. - Marko 11:24
na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake. - I Yohana 3:22
Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe. -Mathayo 26:39
Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. - Mathayo 6:6,7
Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji. - Waebrania 4:16
kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; - Waefeso 6:18
Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano. I Timotheo 2:8
Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua, Naye ataisikia sauti yangu. - Zaburi 55:17
Atakapoyaelekea maombi yake aliye mkiwa, Asiyadharau maombi yao. - Zaburi 102:17
Haleluya. Nampenda Bwana kwa kuwa anaisikiliza Sauti yangu na dua zangu. Kwa maana amenitegea sikio lake, Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote. - Zaburi 116:1,2