Utangulizi:
Kila mwanadamu anayeishi katika hii Dunia Mungu
anampango na yeye tangu kuzaliwa kwake hadi mwisho wa maisha yake, Sasa katika
kuishi ili Mungu akamilishe Mpango wake, Mwanadamu ndani ya Moyo wake Mungu
ameandika maandishi ambayo leo Mungu
amekupa nafasi ya kuyasoma ili kuifahamu hatima yako,Kwa kuwa hatima ya
mwanadamu imefichwa na Mungu ndani ya Moyo wa mwanadamu kazi kubwa ni kuyasoma
maandishi yaliyoandikwa
Bila shaka
unaweza kushangazwa kidogo na kichwa cha somo ila uhalisia wa maisha ya kila
mwanadamu au hatima ya Mtu imeandikwa Moyoni mwake yeye mwenyewe japo sirahisi
kuelewa kama hujapata Neema ya kugunduwa hilo,
NDANI YA MOYO WA MWANADAMU
Jambo
kuu la kufahamu kabla ya mambo yote fahamu kuwa Ndani ya Moyo wako Ndiko makao
makuu ya Wewe (Mwanadamu)
v Ndani
ya moyo ndiko unakotoka ushindi wa jambo lolote unalotaka kufanya
v Ndani
ya Moyo ndiko kunakotokana na kushindwa jambo
v Ndani
ya Moyo ndiko unakotoka Uwoga( kuweza au kushindwa kunatoka ndani)
v Ndani
ya Moyo ndiko unakotoka Ujasiri( kufanya unalotaka kufanya liwe baya au zuri,
v Maamuzi
yote yanaanzi katika Moyo kuuza au kununuwa(kuwowa au kuolewa
v Umasikini
au utajiri unaanzia katika Moyo
v Mikataba
au mipaka ya kila jambo inafanyikia ndani ya Moyo –Mkataba siyo karatasi nikile mlichoridhiana toka ndani ya
miyoyo yenu,
Bibilia
inatundisha nini juu ya Mpango mzima wa Mungu na juu ya Hatima ya maisha yetu
Waefeso
3:11
Mateso ya watu wengi siku za leo kunasababu
zinazosababisha wateseka hivyo haijalishi kuteseka kwa nanma gani, watu
wanafikiri kuwa na fedha nyingi ni kufanikiwa au kuwa na afya ya kimwili ni
kufanikiwa hivyo kila mmoja anajipima kwa kile anacho kiona kwake ni mafanikio,
je hilo lilo lengo la Mungu au kusudi lake hatima yako iwe hiyo na hivyo ulivyo
ndivyo ulivyosoma ndani ya moyo wako,
Uzima wako unatafri halisi hapa Duniani na hata mwisho
wako kwakuwa hakuna Mtu aliyejileta bali ameletwa swali sababu ni zipi za yeye
kuishi,au kusudi la yeye kuwepo ni nini?
Hakuna
atakaye kataa kwamba ndani ya moyo wake kuwa hakuna maandishi
Maandishi
ni nini
Ni
alama inayosomeka kwa kusudi au kwalengo
la kutaarifu au kuagiza Yule anayepaswa
kusoma na kuelewa,
Waefeso 3:11
“…Kwa kadri la kusudi la milele alilolikusudia katika
Kristo Yesu…” Inatufundisha hapa kwamba kila mtu alie hai ana kusudi la milele
limeandikishwa ndani ya moyo (maelekezo yako ndani ya moyo yameandikishwa ili
utakapo kuwa mkubwa, ndio yanatengeneza uwewe na mambo kadha wa kadha), hatma
ya maisha yako inauhusiano mkubwa sana na moyo wako.
Nini maana ya moyo?
Kazi ya moyo ni kupeleka minerals (madini), ndani ya
mwili kupump (kusukuma) oksijeni, mwili mzima na kusukuma uchafu nje ya mwili.
Mara moyo wa mtu utakapo acha kufanya kazi mtu anakufa hapo hapo, sababu moyo
ndiyo centre inayofanya mtu aishi.
Kuna utu wa ndani ya mtu ambao ni roho, na nje ya mtu
ambao ni mwili, na mtu wa ndani (ambaye ni roho) naye ana moyo pia, ndio maana
Mungu ni Roho lakini ana moyo Mwanzo 8:21 “Bwana akasikia harufu ya
kumridhisha; Bwana akasema moyoni sitailaani nchi tena”.
Mwanzo 17:17 “Ibrahimu akaanguka kifudifudi akacheka,
akasema moyoni…” Mwanzo 18:12 “Sara Moyo wake ukacheka Mwanzo 24:45.
Mungu anapotaka kupanda kusudi la maisha ndani ya mtu
hupanda moyoni, ndio maana moyo wa mtu ukiwa mzito mambo yake hayawezi
kufanikiwa, atakuwa anaona uzito katika kila jambo analolifanya.
Mwanzo 27:41, “…Esau akasema moyoni mwake...” Kutoka
4:14 “… naye atakapokuona atafurahi moyoni mwake…”
Kumbukumbu la torati 2:30 “..akamtia ukaidi moyoni
mwake..” tunajifunza unapotiwa ukaidi moyoni mwako, ukaidi huo unajidhihilisha
mwilini, unakuta mtu hupendi kuwa mkaidi, lakini ndio unakuwa ushatiwa ukaidi.
Ndio maana mtu utamsikia anasema nakupenda kutoka moyoni mwangu, hapo cha
kujiuliza je huo moyo anaouzungumzia ni wa kwake, maana watu hutiwa mioyo
tofauti na kusudi la Bwana.
Mithali 4:23 “..linda sana moyo wako kuliko vyote
ulindavyo maana huko ndiko zitokako chemichemi za uzima..” Biblia ya kiingereza
inasema “Keep thy heart with all diligence; for out of it are the issues of
life” Tunajifunza hapa mambo yote za maisha ya mtu huanzia moyoni, matatizo
yanayowakumba watu au mafanikio ya mtu huanzia moyoni mwa mtu, “ISSUES OF LIFE”
Kutoka 35:35 “…Amewajaza watu hao akili za moyoni ili
atumike katika kazi ya kila aina...”
kutoka 35:34 “…nimemtilia moyoni mwake ili apate kufundisha..”
Siku hii ya leo, ninaomba Mungu apande jambo moyoni
mwako, ili kutimiza kusudi la nchi yetu Tanzania. “Utamkuta mtu mwingine
anatenda jambo kwa ufanisi ulio wa juu mpaka watu wanashangaa wanamuuliza hivi
ulisoma wapi, kumbe hata hajasoma lakini ndio kusudi la moyo wake.
Mungu amepanda kitu ndani ya moyo wako ili kupitia kile
uwe na mafanikio, shule haiwezi kukuletea mafanikio, kile kilichopandwa ndani
ya moyo wa mtu ndio mafanikio yake. Ufufuo na Uzima imepandwa ndani ya moyo wa
Yesu, ndio maana hatuhitaji mtu atuelekeze njia ya namna ya kwenenda.
Kumbukumbu 4:9 “..mambo uliyoyaona yakaondoka moyoni
mwako…”, Kumbukumbu 8:2 “…kuyajua yaliyo moyoni mwako…” Hata Mungu kuwapitisha
wana wa Israel jangwani ni ili Mungu ajue yaliyo mioyoni mwao, kama watashika
amri zake ama sivyo.
“Issues za maisha zipo mioyoni mwa mtu” Nataka nianze
biashara, nataka nisome shule, nataka niache kazi vyote hivyo huanzia moyoni.
Moyoni mwangu nikimtumikia Mungu najisikia vizuri, nikimuimbia Mungu njisikia
vizuri, nikimtolea Bwana moyoni mwangu najisikia vizuri sana, ndio maana mtu
anasema nasema kutoka moyoni Mwangu. Na ukisimamia kusudi hilo utafika pale
Mungu alipokukusudia.
Shetani ana tabia ya kuiba mioyo ya watu yenye kusudi la
Mungu, anaandikia maelekezo yake yeye ambayo ni tofauti na maelekezo ya Mungu,
anakutole kusudi la Mungu anaandika maelekezo yake ili uelekee upotevuni,
utasikia najisikia nikaibe kabisa, najisikia niwe mwana mziki, najisikia nivute
bangi, napenda ukahaba, kumbe ndio maelekezo yaliyonakiriwa na shetani ndani ya
moyo wako.
Unakuta mtu alivyokuwa mtoto mdogo, alikuwa anampenda
Mungu, anasema nataka nimtumikie Mungu, niwe mchungaji, niwe mwimbaji, lakini
mtu huyo akishakuwa mtu mzima anakuwa tofauti kabisa “ukiona upo hivyo ujue
umebadilishiwa moyo”.
Unakuta mtu ameokoka anaolewa na mganga wa kienyeji,
mnamuuliza mnamwambia unawaza nini wewe anakwambia Mchungaji nampenda toka
moyoni mwangu, nampenda huyu kaka toka moyoni, ukiangalia kaka mwenyewe ni
mvuta bangi, hata haeleweki. Kumbe moyo wako uliibiwa na shetani na huyo kaka
mvuta bangi akaandikishwa ndani ya moyo wako, bila wewe kujua.
Mtu umeokoka lakini unakuta unampenda binti/kaka wa
kiislamu, kumbe umebadilishiwa moyo, wamenakiri kwenye moyo wako kuwa utaolewa
ana kuoa muislam. Leo tunarudisha mioyo yote uliyobadilishiwa, lazima kusudi la
Bwana litimie, kusudi la Bwana ulilowekewa ndani ya moyo wako tunalirudisha leo
kwa jina la Yesu. “Daudi alisema eeh moyo wangu na vyote vilivyo ndani yangu
mche Bwana”.
Shetani anajua issues zako zote za maisha yako zinatokea
moyoni, kiu yako ya kuimba, kuhudhulia ibadani, kutoa fungu la kumi, kumtumikia
Bwana vyote huanzia moyoni. Shetani ili abadilishe kusudi lako anaiba moyo,
anabadilisha kusudi lililonakiriwa na Mungu moyoni mwako, anaweka maelekezo
yake, unajikuta uliyokuwa unatenda hutendi tena, unaingiwa na kiu ya kutenda
mambo mengine ambayo hujawahi hata kuyawaza. Lakini wewe ukikaa unaona upo
sahihi sababu unachokifanya kinatoka moyoni, kumbe umebadilishiwa moyo ili
uelekee upotevuni.
Kuna watu huwa wanajuta baada ya kutenda jambo,
usiangalie kwamba hili jmbo linatoka moyoni mwangu, cha kufahamu ujue huo moyo
ni wa kwako, unayoyatenda ni kusudi la Bwana tangu awali? Huu ni wakati wa
kukana maelekezo ya moyoni mwako kama sio kusudi la Mungu. Shetani amepanda
jambo ndani ya moyo wako umeanza kulitumikia, kumbe ni kusudi lililopandwa na
shetani.
Shetani akitaka kukuandikia maelekezo yake, huwa lazima
usumbufu utokee, ulikuwa unajiweza vizuri kifedha, ghafla unakosa hela ya kula,
hata hela ya kwenda kanisani huna, kazi unafukuzwa kumbe ni shetani anakuandaa
kukuchomoa kwenye lile kusudi la Mungu, ukishaona umechoka hueleweki shetani
anakuambia hilo sio kusudi lako, anakubadilishia maelekezo yaliyondani mwako
“mara unaalikwa kwenye semina ya “empowerment”, kumbe shetani ndio anakuwa
anakutengeneza kwenye kusudi lake.
Leo ninamlazimisha shetani na watenda kazi wake wote
kurudisha mioyo yenu ya asili irudi kwenu, na moyo wako unarudi kwa jina la
Yesu. Unarudi kwenye kusudi lako la milele.
Namna ya kuomba
Ngo’a maelekezo ya kishetani yaliyopandwa ndani ya moyo
wako ili yakuongoze kwenda mbali na kusudi lako la milele, nayaondoa maelekezo
hayo kwa jina la Yesu. Ninakataa maelekezo yaliyowekwa ndani ya moyo wangu
kugeuza kusudi la Mungu ndani yangu, kama niliandikiwa kuwa muombaji narudisha
kusudi hilo kwangu kwa jina la Yesu, ninakataa kiu ya miziki ya kizazi kipya
ndani yangu, kiu ya uzinzi, kiu zote za kishetani kunipindisha na kusudi langu
la milele nakataa kwa jina la Yesu.
Leo namng’ang’aniza shetani na malaika zake na majini
yake na vibwengo vyake warudishe moyo wako kwa jina la Yesu. Maelekezo ya
kishetani yalioandikishwa ndani ya moyo wangu ili kunipeleka mbali na Mungu
nayakataa kwa Jina la Yesu, maelekezo yaliyonipeleka mbali na baraka zangu naukataa
moyo wenye maelekezo hayo kwa jina la Yesu, anza kudai moyo wako, moyo wa
kumcha Bwana, moyo wa ubunifu, moyo wa mafanikio, moyo wa safari nautaka moyo
wangu kwa jina la Yesu.
Moyo wa kiburi mlioniwekea naukataa kwa jina la Yesu,
moyo wa mauti mlioniwekea naukataa kwa jina la yesu, nautaka moyo wangu kwa
jina la Yesu. Nataka moyo wangu, moyo wa ushindi, moyo wa kushika fedha, moyo
wenye msimamo, moyo unaompenda Yesu, naurudisha moyo wangu katika jina la Yesu
Kristo.
0 comments:
Post a Comment