Utangulizi:
Kila mwanadamu katika maisha yake ya hapa Duniani mbali na mwisho wake bado anayo hatima ya maisha yake Mungu aliyomkirimia au kumjali hilo ndilo analolisumbukia kila inapoitwa siku, na wengi hatima zao hizo zimepindishwa na Muovu Bila wao kujuwa au kwa kutojuwa lakini wakakosa msaada katika somo hili ninataka nikurudishe katika ile hatima yako iliyopindishwa katika jina la yesu,
Hatima katika maisha ni nini?
Hatuwezi kujifunza hapa bila kujuwa maana ya kile ninachokiongelea Hatima Ni Hali au uwezo Wa mtu kufikia katika mipango au malengo yake kama alivyoiona au kupanga moyoni mwake, maisha ni ule uwepo wa uhai wa kiumbe chochote amacho kipo katika hii Dunia, sasa uhai wako unaambatana na mahitaji yako ili huu uhai uendelee kuwepo hadi kufikia kusudio la Mungu, kila kiumbe chenye Uhai kina mahitaji yanayo hitajika, hiyo ndioinafaya mipango iwepo ili kufikia ile hatima,
Mithali 16:1 Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana.haya maandaliyo ya moyo ni mipango ya hatima yako kumbuka katika moyo ndiko Roho mtakatifu anapaswa kukaa na ndiko karakana ya kuunda kila unachokitaka kitokee,
Kitabu cha Petro ni waraka wake kwa watu wote; ukisoma, 2 Petro 1:3 “kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe.
Neno la Mungu linamaanisha kuwa uweza wa Mungu umetupatia vitu vyote, kwa kumjua yeye. Kumbe hapa tunapata kujua kuwa ni mapenzi ya Mungu tuwe na vitu vyote, na uweza huo wa Kiungu umeshatupa tayari kila kitu kitupasacho kuishi.
Tunajifuna hapa nini kabla ya maisha yetu kuanza Mungu alikuwa ameshatukirimia mambo yote. Yaani Hatima ya maisha yako Ukisoma Yeremia 1:4 “kisha neno la bwana likanijia Yeremia…” Biblia inapotaja neno inamaanisha “Mungu” kwasababu katika (Yohana 1:1-5) Biblia inathibitisha kuwa neno hilo ni Mungu mwenyewe. Yesu Kristo ndio neno lililokuwa linawajia manabii hapo kabla,
Tunajifuna hapa nini kabla ya maisha yetu kuanza Mungu alikuwa ameshatukirimia mambo yote. Yaani Hatima ya maisha yako Ukisoma Yeremia 1:4 “kisha neno la bwana likanijia Yeremia…” Biblia inapotaja neno inamaanisha “Mungu” kwasababu katika (Yohana 1:1-5) Biblia inathibitisha kuwa neno hilo ni Mungu mwenyewe. Yesu Kristo ndio neno lililokuwa linawajia manabii hapo kabla,
Hivyo kwa kuwa Yesu ndiye Neno tunaweza kusema kwamba Yesu alipomjia Yeremia akamwambia, (Yeremia 1:5) “kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa;” Kumbe Yesu alimjua Yeremia kabla ya kuumbwa tumboni. Kimsingi, Hakuna mtu ambaye anaweza kukumbuka kipindi yupo tumboni wala kabla ya kuwa tumboni,wakati mwingine hata mama mjaamzito kuna wakati siku zinamchenga siku ya yeye kupata Mimba ila Mungu hachengwi kwa jambo lolote,
Mungu alikujua kabla ya kuwepo tumboni na alikukirimia vitu vyote. Swali la kujiuliza wewe mwenyewe hapo ulipo kama Mungu alikujua tangu huko mwanzo, Tumboni mwa Mama yako na alikukirimia kila kitu yaani akakupatia hatima yako yote kwanini maisha yako bado yapo hivyo yalivyo sasa,?
Hapo ndipo Utakubaliana na Mimi ya kwamba Hatima yako imepindishwa,Japo si rahisi kulifahamu hili ila maandiko matakatifu ya tatusaidia kujuwa Hatima yetu imepindishwa wapi,imepindishwa vipi na nani? Tuangalie maandiko
Muhubiri 10:7 Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi, na wakuu wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa.
Kumbe hatima ya mtu kupindishwa haijalishi wewe unacheo gani ua umesoma kiasi gani hapa wakuu wanaostahili wanatembea na miguu watumwa wanafurahia juu ya farasi, ndivyo maisha unayoyaishi maisha yako unayostahili hauyaishi wanaishi watu wengine wasiyostahili na wewe unaendelea kutaabika,
Tukirudi kwa habari ya Yeremia, Mungu aliongea na Yeremia akiwa kijana mdogo kuwa yeye amewekwa kuwa nabii wa mataifa (Yeremia 1:5).
Kumbe kabla hujazaliwa Mungu alikwishakuweka katika njia ya Hatima ya maisha yako kama Yeremia; Jiulize nini kimetokea hadi leo upo kwenye njia nyingine? Mungu alikuwekea mafanikio tangu mwanzo, lakini jiulize nini kimetokea hadi leo upo katika hali hiyo isiyoeleweka hata na wewe mwenyewe?
Kuna watu maisha yanawachanganya hadi wao wenyewe wanashindwa kujielewa kwanini wapo hapa Duniani, hii inawapelekea hata wengine kukatatamaa,
Yawezekana wewe ni maskini leo, lakini unatakiwa ujue pia Mungu hakuiti kwa jina la umaskini bali anakuita kwa jina ambalo ndilo Hatima yako.
Yawezekana wewe ni maskini leo, lakini unatakiwa ujue pia Mungu hakuiti kwa jina la umaskini bali anakuita kwa jina ambalo ndilo Hatima yako.
Japo inanisikitisha sana kwa Yule mtu anayesema kuwa eti! amekubali Matokeo ya yeye kuishi katika maisha anayoyaishi, si mpango wa Mungu wewe utaabike na wala Yesu hakuwa masikini kama vile watu wengine walivyo karirishwa kama yesu alikuwa masikini uwezo wakulisha watu Maalfu kwa maalfu aliutoa wapi ni masikini Gani mwenye uwezo huo,
Warumi 8:29-30 “maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.
Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita na wale aliowaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki, hao akawatukuza” kumbe tunaona kuwa Mungu amekwisha kuchagua tangu asili na tangu asili Hatima yako inaongelewa naMungu.
Na ukisoma mipango ya Mungu juu yako, hutaona kuwa unatakiwa kuishi hivyo unavyoishi kwa kuharibu mimba, au matatizo ya ndoa, au mateso ya umaskini, au kutokufanikiwa au magonjwa ambayo yanayokusumbua sasa. Kukataliwa katika jamii Yeremia 29:11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.
Hivyo mwanzo mwisho Mungu anakujuwa na kukujali na Hatima ya maisha yako iko pale pale Inawezekana ulitakiwa kuwa Mbali sana ki-Roho na kimwili ila hatima yako imepindishwa na yule muovu, kwamaslahi yake
Kuna mambo makuu na makubwa ambayo Mungu anakuwazia katika maisha yako lakini hayajakamilika kwasababu njia uliyotakiwa kupita imekwepeshwa
(Waefeso 3:20 Malaika alipomtokea Gideoni alimwita kwa jina la “shujaa”. Japokuwa Gideoni alikuwa mtu wa kawaida kwa wakati ule bado kumbe tangu tumboni aliitwa shujaa na alitakiwa kuwa shujaa. Tatizo ni maisha yaliyomzunguka yalimfanya asiujue ukweli huu kuwa yeye ni shujaa. Hata wewe maisha yaliyokuzunguka yanakufanya usijitambuwe kuwa hatima yako ni ipi na wewe ni nani kilingana na Hatima yako,
Pamoja na yote jina lile halikubadilika mbele za Mungu kuwa yeye katika ulimwengu wa roho anaitwa shujaa. Je wajua kuwa kabla ya kuzaliwa ulikuwa kwenye mapafu ya Mungu yaani ulikuwa pumzi ya Mungu, ulikuwa pamoja na Mungu ndio maana biblia inakuita “mwana wa miungu” (Zaburi 82:6),
hiyo ndio asili yako. Rudi kwenye asili yako leo, asili yako sio uzinzi na uasherati, sio madeni, sio magonjwa, sio kushindwa. Amua kurudi kwenye asili yako kwasababu tupo duniani Kwa kusudi la Mungu “mpango” huwezi kufa ukiwa kwenye njia ya Mungu mpakamipango yako ikamilike, wakunyweshe sumu wakuloge hutokufa mpaka ukamilishe Hatima yako.
Kuna watu, kwasababu ya maisha wanayopitia wamejikuta wakijiuliza kuwa Mungu yupo kweli? Unawaza kama Mungu angekuwepo usingepitia kwenye mateso yako? Ni muhimu kujua Mungu alishakukirimia vitu vyote tatizo ni kwamba watu wengi hawapo katika asili yao.na hatima yao ilisha pindwa
Kuna watu, kwasababu ya maisha wanayopitia wamejikuta wakijiuliza kuwa Mungu yupo kweli? Unawaza kama Mungu angekuwepo usingepitia kwenye mateso yako? Ni muhimu kujua Mungu alishakukirimia vitu vyote tatizo ni kwamba watu wengi hawapo katika asili yao.na hatima yao ilisha pindwa
Biblia inasema Mungu ametukirimia vyote kwa kumjua yeye, sasa unachotakiwa kufanya ni kurudi katika njia, kwa kuanza
· kusoma neno,
· kufanya maombi yaani unatakiwa ubadilishe staili yako ya maombi na uhamie kwenye maombi ya kushindana ili kurudisha asili ya maisha yako.
Waefeso 6:12 Omba Kwa kushindana Na falume yaani serekali ya Nguvu za Giza,
Kuna mashetani na wachawi ambao wapo katika ulimwengu wa roho ili kubadili Hatima yako ambayo Mungu alikuwekea ili uiishi. Inawezekana Mungu alikuweka kuwa kiongozi mkubwa na mwenye kukubalika
lakini wachawi na mashetani waweza kukuhamisha kutoka katika njia ya Mungu aliyokuitia. Amua kurudi katika Hatima yako ambayo Mungu alikuita kwayo.
Warumi 8:19-21 Yaani hata viumbe vinavyoishi duniani vimetiishwa chini ya uharibifu yaani vimehamishwa kutoka katika asili yao. Viumbe navyo vyajua kuwa havipo katika asili yake, ndio maana navyo vinatarajia kufunuliwa kwake Kristo Yesu ili virudi katika asili yao.
Warumi 8:19-21 Yaani hata viumbe vinavyoishi duniani vimetiishwa chini ya uharibifu yaani vimehamishwa kutoka katika asili yao. Viumbe navyo vyajua kuwa havipo katika asili yake, ndio maana navyo vinatarajia kufunuliwa kwake Kristo Yesu ili virudi katika asili yao.
Hata Hana aliposumbuka miaka mingi pasipo kupata mtoto alimwomba BWANA akasema ukinipa mtoto atakuwa mjakazi wako, hapo ndipo Mungu alipomuingiza nabii Samweli kwenye tumbo la Hana. (1Samweli 1:11) Nabii Samweli ni nabii aliyekuwa na nguvu za Mungu, ambaye Mungu alimtumia sana; kumbe asili yake ni ile iliyotajwa na Hana akiwa kwenye maombi kabla hata ya Samweli kuzaliwa. Amini usiamini maisha unayoishi, sio ambayo Mungu alikupangia wewe uishi; hata wewe mwenyewe ni shahidi kuwa maisha hayo siyo uliyotaka kuishi.
Kuna mashetani wamepindisha asili yako na kukupa maisha mengine na bahati mbaya zaidi umekubali maneno ya watu kukwambia “vumilia vumilia”. Kuna muda unatakiwa uamue kuchukua hatua ya kupambana ili urudi kwenye asili yako.
Ndio maana watu ambao hawachukui hatua ya kuomba maombi ya Kupambana wanajikuta wanahama kila kanisa bila mafanikio kumbe unatakiwa ufanye maamuzi ya kushindana na falme za giza. Huu ni wakati wa kuamua kurudi kwenye asili yako uliyopangiwa na Mungu.
Sikuzote shetani hufanya vita na watu ambao tangu asili waliitiwa maisha mazuri, yeye (shetani) huwahamisha na kuwafanya wawaze kuwa wanavyoishi sivyo Mungu anavyowataka waishi.
Sikuzote shetani hufanya vita na watu ambao tangu asili waliitiwa maisha mazuri, yeye (shetani) huwahamisha na kuwafanya wawaze kuwa wanavyoishi sivyo Mungu anavyowataka waishi.
Leo amua kurudi katika asili yako, pambana na mamlaka za giza. Imeandikwa kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama bali ni juu ya falme na mamlaka za giza. Kataa kuishi maisha hayo na uamue kurudi kwenye asili yako aliyokupangia Mungu. Mungu hakukupangia mateso hayo unayopitia,
Popote ulipo kama Umeshiriki somo hili niwakati wako mzuri wa kuanza kuomba maombi ya kupambana kama maandiko yanavyo sema
Kubukumbu 1:7 Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;
Na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako.
Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani.
Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako.
Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo. Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. Fanya maombi Yakurudishwa katika hatima yako
Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani.
Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako.
Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo. Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. Fanya maombi Yakurudishwa katika hatima yako
Waefeso 6:12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Mungu akubariki sana wewe kushiriki somo hili pia limefafanuliwa zaidi katika DVD Ukihitaji somo hili linapatikana madukani na pia ikiwa hazijakufikia hapo ulipo piga simu kuagiza utatumiwa na utatazama na kusikiliza chumbani kwako, na utapata nafasi ya kushiriki maombi ya kurudisha hatima piga simu uagize Nakala yako
1. DVD HATIMA ILIYOPINDISHWA
2. DVD UPENYWE WA KUMILIKI
3DVD SIRI KUU 3 ZAKUTUZA SIRI ZAKO ZOTE
0756 809 209/0653 294219/0786608801
Kwa Mtumishi wa Mungu,Samson o Mboya