Thursday, December 12, 2013
Baada ya miuujiza mikubwa kutendeka ndani ya Hema ya kinabii, wananchi kwa furaha kubwa wakishangilia na matawi kutoka kila kona. ya kinabii
8:52 AM
No comments
Hatimaye nyankumbu mkoni Geita yageuka kuwa kisima cha baraka ,baada ya wanakijiji wa nyankumbu kushangazwa na matendo makuu ya Mungu pale mabubu wawili walipoongea!Jambo hili lilitokea baada ya maombezi ya mtu wa Mungu nabii Samson.
Wednesday, December 11, 2013
Maombi katika Hema ya Kinabii na Nabii Samson,
12:09 PM
No comments
Maombi Uponyaji Kufunguliwa, Ungana na Mamia ya watu wanaokujaa kila siku Katika Hema Y akinabii Kukutana na Mtu wa Mungu Nabii Samson kwaajili ya maombi na maombezi sasa umbali kwako kisiwe kikwazo unaweza kumpigia simu na akakusaidia, piga sasa 0756 809 209 kwa ushahuri na Maombi maalumu,
Anusurika kufa
11:58 AM
No comments
Bibi akielezea yaliyomsibu Na Mtu wa Mungu Nabii kulia akisikiliza kwa Umakini Mkubwa kabla ya ya Kuombewa,
Yaliyoshindikana kwa wasomi Mungu anayawza Yote
11:44 AM
No comments
Mtu wa Mungu Nabii Samson Akuchukuwa Maelezo kamili kutoka kwa DR Mstaafu kwaajili ya Kumfanyia Maombi ya Kufunguliwa, Pale pale katika Hema ya Kinabii, Nyankumbu Geita hapa hapa nchini Tanzania
Mtumishi wa Mungu Mwinjilisti Stivin O mboya wa Morogoro akiwa na Ndugu yake Nabii Samson Mboya
10:34 AM
1 comment
Mpakwa mafuta wa Mungu Hatimaye aingia Ndani ya Jiji la Geita kwaajili ya kuhudumu Katika Hema ya kinabii Furaha yatawala kati ya wana ndugu Hawa, kwa Historia Fupi Hii ni Familia ya kikuhani Uzao wote Bwana ameuita umtumikie,
Ibada Maalumu ya Meza ya Bwana iliyofundishwa na Mtu wa Mungu
10:19 AM
No comments
Mtu wa Mungu akiwa na Mke wake Mpezi wakati anafundisha Nguvu iliyoko katika Kushiriki meza ya Bwana
Nahitaji Neno la Kinabii kutoka kwa mtu wa Mungu 0756 809 209
10:11 AM
1 comment
Yule Mtu wa Mungu Nabii Samson Akiombea Picha ya Mtu aliyekuwa amepotea siku Nyingi Na hatimaye Kwa ushuhuda Mkubwa Aliyepotea akarudi ,Ikiwa kunatatizo lina kutatiza Mungu analiweza Yaliyoshindikana kwa wanadamu Kwa Yesu Yanawezekana Umbali usiwe kikwazo kwako Mpigie simu hudumu ni Bure 0756 809 209 Maisha yako hayatabaki kama yalivyo sasa,
Wana wa Manabii wakiwa na Mwalimu wao katika Hema ya Kinabii pale pale Nyankumbu-Geita Tanzania
9:57 AM
No comments
wana wa manabii Katika Hema ya Kinabii pale Nyankumbu Mkoa mpya wa Geita Tanzania wakiwa katika Mafundisho Maalumu, ya watoto,
Babu aliyebahatika kubadilisha maisha yake baada ya kukutana na Yule Mtu wa Mungu
9:44 AM
No comments
Pichani ni Babu anaonyesha Furaha yake Baada ya kukutana na Mtu wa Mungu Nabii Samson Uso kwa uso,Ghala maisha yake yalifunguliwa na kuwekwa huru Baada ya mateso ya siku nyingi,
Friday, December 6, 2013
Ungana na Mamia ya watu kwaajili ya ukombozi na kufunguliwa Ndani ya Hema Ya kinabii,
1:46 PM
No comments
Umbali kwako kisiwe kikwazo Kuhudumiwa Piga simu kwa Ushahuri na Maombi Utaongea na Mtu wa Mungu Nabii Samson Live Naye atakuhudumia Ni Bure masaa 24 siku saba za juma piga sasa 0756 809 209 au 0653 294219 au Ukiwa kanda ya ziwa fika pale kanisani Nankumbu katika Hema ya Kinabii Geita Utahudumiwa, haraka sana,
Grace akiwa na Mpambe wake Miss Talent,
1:34 PM
No comments
Grace Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Sauti Baada ya kuwasili Mji wa Dhahabu Geita Alipata Muda mzuri wa Kukutana na Ndugu Jamaa Na Marafiki alikuwa Na machache ya kusema Kama unavyojuwa Wasomi Hawaongei sana alishukuru Wazazi Baba Na Mama Ndugu Jamaa na Marafiki akawakaribisha Katika Chakula cha jioni,
Nifanye Nini Maombi Yangu Yajibiwe?
1:22 PM
No comments
ili Maombi yako yajibiwe haraka
Utangulizi:
Maisha ya mkristo ni zaidi ya kuishi na kule anakokufikiria yeye,
kila
mmoja anaishi kwa fikira za Akili alizope na Mungu na kwa mipango ilyopo moyoni mwake na kwa imani
iliyondani ya Moyo wake akiaamini kwamba anayetowa reziki zote na
baraka ni Mungu, hili halikataliwi na Mtu,
japo
watu wanahitaji kufanikiwa bila kanuni au utaratibu uliyowekwa na
mwenyewe anayebariki, kutaka kibali mbele za Mungu kinyume cha utaratibu
na kanuni alizoziweka Mungu ni kama kuvuna katika shamba ambalo wewe
hukushughulika na jambo lolote zaidi ya kuvuna,
kwa lugha nyingine kutaka kituambachohujakifanyia kazi ni si vizuri kwakuwa hata Neema tumepewa kwa kuikubali na kuipokea,
waefeso 1:1
kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.
Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake.
Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa.
Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.
Naye alituzidishia hiyo katika hekima yote na ujuzi;
akiisha kutujulisha siri ya mapenzi yake, sawasawa na uradhi wake, alioukusudia katika yeye huyo.
Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.
Naye alituzidishia hiyo katika hekima yote na ujuzi;
akiisha kutujulisha siri ya mapenzi yake, sawasawa na uradhi wake, alioukusudia katika yeye huyo.
Yaani,
kuleta madaraka ya wakati mkamilifu atavijumlisha vitu vyote katika
Kristo, vitu vya mbinguni na vitu vya duniani pia. Naam, katika yeye
huyo;
na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.
kuishi kwetu
kunahitaji maelekezo ya kila siku yaani kumuomba Mungu atufundishe namna
ya kuishi tuwapo hapa Duniani ili kwenda sawa sawa na mpango wa Mungu,na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.
wengi wetu tumebadilisha Maelekezo tuliyopewa na Mungu, baada ya kuishi vile anavyotaka tunaishi vile tunavyotaka sisi na kuanza kumlazimisha Mungu aingie katika mawazo yetu,
Tamani kuingia katika mawazo ya Mungu Usimlazimishe Mungu Kuingia Katika Mawazo Yako,
Maandiko Matakatifu kutoka katika kitabu kilichoandikwa na Mathayo 6:33
Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.
Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.
Mungu
hakututuma au kutuagiza kutafuta chakula na kitu cha kunywa bali
maagizo ni kutafuta Ufalme wake mengine Tutazidishiwa Kwa lugha nyepesi
sisi tunavyokuwa waaminifu kuutafuta ufalme wake yeye ana hakikisha
hatuishiwi kwa jambo lolote lile,
Katika haya yote nidhamu inahitajika sana kwa Mungu na kwa wanadamu wote,
Kumjuwa
Mungu Si tatizo kwa watu siku za leo au Kuwa na imani si tatizo kwa
watu siku za leo ila imani na kutokuamini ni vitu wiwili tofauti,
unaweza kuwa na imani lakini imani uliyo nayo huiamini japo unayo,
kumjuwa
Mungu ni habari nyingine na kumwamini Mungu ni hatuwa ninyinge ,hili
linawasumbuwa sana watu wengi Mungu atusaidie sana ,
Amesema Tuutafute ufalme wake yeye si muongo Tufanye hivyo, tena kwa uhakika maandiko Matakatifu yanakazia katika kitabu cha
Mathayo 7:7
Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;
kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.
kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.
Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe?
Au akiomba samaki, atampa nyoka? Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?
Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.
Au akiomba samaki, atampa nyoka? Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?
Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.
hii inamaanisha tangu kipindi kile cha agano la kale hata sasa Mungu alikuwa ni wautaratibi,
Yeremia29:13/mithali 14:2,ufunuo 13:1.timotheo 1:7 mithali 13:18
Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.
Nami nitaonekana kwenu, asema Bwana, nami nitawarudisha watu wenu waliofungwa, nami nitawakusanya ninyi, nikiwatoa katika mataifa yote, na katika mahali pote, nilikowafukuza, asema Bwana; nami nitawaleta tena, hata mahali ambapo kutoka hapo naliwafanya mchukuliwe mateka.
Nami nitaonekana kwenu, asema Bwana, nami nitawarudisha watu wenu waliofungwa, nami nitawakusanya ninyi, nikiwatoa katika mataifa yote, na katika mahali pote, nilikowafukuza, asema Bwana; nami nitawaleta tena, hata mahali ambapo kutoka hapo naliwafanya mchukuliwe mateka.
Kupata kibali kunazuiliwa na mambo mengi sana kwakuwa mawasliano siku zote yanaazia hatuwa ya kwanza kwenda hatuwa ya pili,
Fuatilia hatuwa chache zitakazo kusaidia wewe kupata kibali
- Tunatakiwa kujifundisha namna ya kujiadabisha sisi wenyewe kabla ya kuwaadabisha wengine,katika maisha yetu ya kila siku
- Mahusiano yako na Mungu yanatakiwa kuongezeka kila siku na si kupunguwa kwa Maovu unayotenda kwa kusudia au kwakutokusudia
- Mahusiano yako na familia/jamii iliyokuzunguka yanamaana kubwa sana Mbele za watu na Mbele za Mungu unayemwamoni na kuyafuata maagizo yake
- Mahusiano ya wewe yanatokana na ukaribu wa wewe kushiriki ibada au mafundisho
- Ushahidi kwa kila mmoja juu ya maisha yako ya kila siku
- Mazingira au maeneo yako ya kutafutia riziki au unakoishi unaishije
Msaada namna ya kutumia somo hili unalolisoma sasa hivi
- Tenga muda wa maombi na kumtafakari Mungu kwa kikubwa au kidogo ulichopata
- ishi maisha ya toba kila wakati kwakuwa hujui saa wala siku ya Yesu kurudi
- Nawezaje kuwa mtakatifu? zaburi 119:11
- Katika familia usiogopo kuwachapa watoto kisa unataka kujionyesha ni mtakatifu hapana juu ya watoto wanatakiwa wakikosea wachapwe Mithali 23:13,mithali 29:17
- Yapo mengi ninaomba haya machache anza nayo kwaza Mathayo 5:6 sisi ni Nuru usikubali kupotesa mwangaza bwana aliyouweka juu yako,
- Ikiwa unahitaji masomo ya Nabii Samson Mungu amemwita katika Umri Mdogo sana Lakini Mungu amempaka Mafuta kuwafunguwa watu katika vifungo Mbalimbali Mungu Anamtumia katika Ishara ya matendo makuu ya Mungu na Miujiza Mingi sana ikiwa unahitaji ushahuri au maombi piga simu yake Utahudumiwa na yeye mwenyewe ni bure kabisa huduma hii piga sasa Nabii samson 0756 809 209
Kutana Live Na yule Mtu wa Mungu Nabii Samson Katika Hema ya kinabii
1:07 PM
No comments
Ukitaka kujifunza Kumwabudu Mungu Katika Roho Na Kweli Fika pale Nyankumbu Geita ikipata nafasi ya Kushiriki ibada Mmoja Maisha yako Hayatabaki Hivyo yalivyo, hii ilikuwa ni ibada Maalumu ya Kuabudu na kusifu Tu, Katika kanisa la Hema ya Kinabii Nyankumbu,
Mtu wa Mungu akiandamana na watumishi wa Mungu kumpongeza Muhitimu
12:51 PM
No comments
Mwalimu wa masomo Maalumu ya kidini Ml Mariki akiambatana na Mke wake Kipenzi kwenda kumpongeza Mtoto wa Mchungaji Mwezao Aliyehitimu Digree yake ya kwaza katika Chuo kikuu cha Sauti Jijini Mwanza, na Kisha sherehe kufanyikia Mkoani Geita Katika Kanisa la Hema ya Ushindi Pale Kagera, Kwa Mchungaji Jonson Jackson (JJP)Mbele kabisa ya Huu Msafara unaouona ni Mke wa Mtu wa Mungu Nabii Samson, Kama walivyopangana Hakika walipendeza sana watu Hawa,
Nasi kwa pamoja team nzima ya Hema ya kinabii Tunaungana na furaha ya Ndugu yetu Mpenda kwa Kumwambia Dada Grace Hongera Sana Tena Sana Mungu akuongezee Bidii ill Uendelee Mbele Usiishie Digree Moja Soma hadi ufikie Uprofesa Inawezekana kabisa, amina,
Nasi kwa pamoja team nzima ya Hema ya kinabii Tunaungana na furaha ya Ndugu yetu Mpenda kwa Kumwambia Dada Grace Hongera Sana Tena Sana Mungu akuongezee Bidii ill Uendelee Mbele Usiishie Digree Moja Soma hadi ufikie Uprofesa Inawezekana kabisa, amina,
Mtu wa Mungu katika Sherehe ya Kumpongeza Mtoto wa Mchungaji Jonson Jackson (jjp)
12:33 PM
1 comment
Nabii Samson aliomwa Kusema Neno la Kinabii Juu ya Muhitimu, Mtumishi wa Mungu aliyepewa Neema Kubwa Ya kuwarejesha watu Kwa Mungu , alinukuliwa akisema Mwenye Hekima ana huzuni sana kwa Hekima aliyonayo na Mtu anayeongeza Maarifa anaongeza masikitiko,
japo Mungu Mbele yetu ametuwekea Mambo makuu mawili kufurahi na kuhuzunika ,ili wakati wakufurahi tuweze kufurahi ila wakati wa mateso tusilie bali tuweze kufikiria tumia Ufahamu wako kufikiria unapokutana na ugumu wowote ule,
na cha kuzingatia fahamu Tu kwamba kila unapoongeza nafasi Moja ya furaha ujue umeongeza pia na nafasi Moja ya Huzuni, Neema ya bwana wetu Yesu kristo ikuongoze maishani Amina,
japo Mungu Mbele yetu ametuwekea Mambo makuu mawili kufurahi na kuhuzunika ,ili wakati wakufurahi tuweze kufurahi ila wakati wa mateso tusilie bali tuweze kufikiria tumia Ufahamu wako kufikiria unapokutana na ugumu wowote ule,
na cha kuzingatia fahamu Tu kwamba kila unapoongeza nafasi Moja ya furaha ujue umeongeza pia na nafasi Moja ya Huzuni, Neema ya bwana wetu Yesu kristo ikuongoze maishani Amina,
Pastor Jonson Jackson (JJP) Kwa pamoja wakimpongeza Mtoto wao Grace Jonson
12:13 PM
No comments
Pastor Jonson na Mkewe Mpenzi aliyezoweleka kwa jina la Miss world Kwa pamoja wakisherekea kwa Furaha kubwa kwaajili ya Mtoto wao mpendwa Grace Joson Kwa Kuhitimu Digree yake ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Sauti kilichopo Jiji la Mawe Mwanza
Mtu wa Mungu Nabii Samson Alialikwa katika hafla hii,
MAANDISHI NDANI YA MOYO
5:34 AM
No comments
Utangulizi:
Kila mwanadamu anayeishi katika hii Dunia Mungu
anampango na yeye tangu kuzaliwa kwake hadi mwisho wa maisha yake, Sasa katika
kuishi ili Mungu akamilishe Mpango wake, Mwanadamu ndani ya Moyo wake Mungu
ameandika maandishi ambayo leo Mungu
amekupa nafasi ya kuyasoma ili kuifahamu hatima yako,Kwa kuwa hatima ya
mwanadamu imefichwa na Mungu ndani ya Moyo wa mwanadamu kazi kubwa ni kuyasoma
maandishi yaliyoandikwa
Bila shaka
unaweza kushangazwa kidogo na kichwa cha somo ila uhalisia wa maisha ya kila
mwanadamu au hatima ya Mtu imeandikwa Moyoni mwake yeye mwenyewe japo sirahisi
kuelewa kama hujapata Neema ya kugunduwa hilo,
NDANI YA MOYO WA MWANADAMU
Jambo
kuu la kufahamu kabla ya mambo yote fahamu kuwa Ndani ya Moyo wako Ndiko makao
makuu ya Wewe (Mwanadamu)
v Ndani
ya moyo ndiko unakotoka ushindi wa jambo lolote unalotaka kufanya
v Ndani
ya Moyo ndiko kunakotokana na kushindwa jambo
v Ndani
ya Moyo ndiko unakotoka Uwoga( kuweza au kushindwa kunatoka ndani)
v Ndani
ya Moyo ndiko unakotoka Ujasiri( kufanya unalotaka kufanya liwe baya au zuri,
v Maamuzi
yote yanaanzi katika Moyo kuuza au kununuwa(kuwowa au kuolewa
v Umasikini
au utajiri unaanzia katika Moyo
v Mikataba
au mipaka ya kila jambo inafanyikia ndani ya Moyo –Mkataba siyo karatasi nikile mlichoridhiana toka ndani ya
miyoyo yenu,
Bibilia
inatundisha nini juu ya Mpango mzima wa Mungu na juu ya Hatima ya maisha yetu
Waefeso
3:11
Mateso ya watu wengi siku za leo kunasababu
zinazosababisha wateseka hivyo haijalishi kuteseka kwa nanma gani, watu
wanafikiri kuwa na fedha nyingi ni kufanikiwa au kuwa na afya ya kimwili ni
kufanikiwa hivyo kila mmoja anajipima kwa kile anacho kiona kwake ni mafanikio,
je hilo lilo lengo la Mungu au kusudi lake hatima yako iwe hiyo na hivyo ulivyo
ndivyo ulivyosoma ndani ya moyo wako,
Uzima wako unatafri halisi hapa Duniani na hata mwisho
wako kwakuwa hakuna Mtu aliyejileta bali ameletwa swali sababu ni zipi za yeye
kuishi,au kusudi la yeye kuwepo ni nini?
Hakuna
atakaye kataa kwamba ndani ya moyo wake kuwa hakuna maandishi
Maandishi
ni nini
Ni
alama inayosomeka kwa kusudi au kwalengo
la kutaarifu au kuagiza Yule anayepaswa
kusoma na kuelewa,
Waefeso 3:11
“…Kwa kadri la kusudi la milele alilolikusudia katika
Kristo Yesu…” Inatufundisha hapa kwamba kila mtu alie hai ana kusudi la milele
limeandikishwa ndani ya moyo (maelekezo yako ndani ya moyo yameandikishwa ili
utakapo kuwa mkubwa, ndio yanatengeneza uwewe na mambo kadha wa kadha), hatma
ya maisha yako inauhusiano mkubwa sana na moyo wako.
Nini maana ya moyo?
Kazi ya moyo ni kupeleka minerals (madini), ndani ya
mwili kupump (kusukuma) oksijeni, mwili mzima na kusukuma uchafu nje ya mwili.
Mara moyo wa mtu utakapo acha kufanya kazi mtu anakufa hapo hapo, sababu moyo
ndiyo centre inayofanya mtu aishi.
Kuna utu wa ndani ya mtu ambao ni roho, na nje ya mtu
ambao ni mwili, na mtu wa ndani (ambaye ni roho) naye ana moyo pia, ndio maana
Mungu ni Roho lakini ana moyo Mwanzo 8:21 “Bwana akasikia harufu ya
kumridhisha; Bwana akasema moyoni sitailaani nchi tena”.
Mwanzo 17:17 “Ibrahimu akaanguka kifudifudi akacheka,
akasema moyoni…” Mwanzo 18:12 “Sara Moyo wake ukacheka Mwanzo 24:45.
Mungu anapotaka kupanda kusudi la maisha ndani ya mtu
hupanda moyoni, ndio maana moyo wa mtu ukiwa mzito mambo yake hayawezi
kufanikiwa, atakuwa anaona uzito katika kila jambo analolifanya.
Mwanzo 27:41, “…Esau akasema moyoni mwake...” Kutoka
4:14 “… naye atakapokuona atafurahi moyoni mwake…”
Kumbukumbu la torati 2:30 “..akamtia ukaidi moyoni
mwake..” tunajifunza unapotiwa ukaidi moyoni mwako, ukaidi huo unajidhihilisha
mwilini, unakuta mtu hupendi kuwa mkaidi, lakini ndio unakuwa ushatiwa ukaidi.
Ndio maana mtu utamsikia anasema nakupenda kutoka moyoni mwangu, hapo cha
kujiuliza je huo moyo anaouzungumzia ni wa kwake, maana watu hutiwa mioyo
tofauti na kusudi la Bwana.
Mithali 4:23 “..linda sana moyo wako kuliko vyote
ulindavyo maana huko ndiko zitokako chemichemi za uzima..” Biblia ya kiingereza
inasema “Keep thy heart with all diligence; for out of it are the issues of
life” Tunajifunza hapa mambo yote za maisha ya mtu huanzia moyoni, matatizo
yanayowakumba watu au mafanikio ya mtu huanzia moyoni mwa mtu, “ISSUES OF LIFE”
Kutoka 35:35 “…Amewajaza watu hao akili za moyoni ili
atumike katika kazi ya kila aina...”
kutoka 35:34 “…nimemtilia moyoni mwake ili apate kufundisha..”
Siku hii ya leo, ninaomba Mungu apande jambo moyoni
mwako, ili kutimiza kusudi la nchi yetu Tanzania. “Utamkuta mtu mwingine
anatenda jambo kwa ufanisi ulio wa juu mpaka watu wanashangaa wanamuuliza hivi
ulisoma wapi, kumbe hata hajasoma lakini ndio kusudi la moyo wake.
Mungu amepanda kitu ndani ya moyo wako ili kupitia kile
uwe na mafanikio, shule haiwezi kukuletea mafanikio, kile kilichopandwa ndani
ya moyo wa mtu ndio mafanikio yake. Ufufuo na Uzima imepandwa ndani ya moyo wa
Yesu, ndio maana hatuhitaji mtu atuelekeze njia ya namna ya kwenenda.
Kumbukumbu 4:9 “..mambo uliyoyaona yakaondoka moyoni
mwako…”, Kumbukumbu 8:2 “…kuyajua yaliyo moyoni mwako…” Hata Mungu kuwapitisha
wana wa Israel jangwani ni ili Mungu ajue yaliyo mioyoni mwao, kama watashika
amri zake ama sivyo.
“Issues za maisha zipo mioyoni mwa mtu” Nataka nianze
biashara, nataka nisome shule, nataka niache kazi vyote hivyo huanzia moyoni.
Moyoni mwangu nikimtumikia Mungu najisikia vizuri, nikimuimbia Mungu njisikia
vizuri, nikimtolea Bwana moyoni mwangu najisikia vizuri sana, ndio maana mtu
anasema nasema kutoka moyoni Mwangu. Na ukisimamia kusudi hilo utafika pale
Mungu alipokukusudia.
Shetani ana tabia ya kuiba mioyo ya watu yenye kusudi la
Mungu, anaandikia maelekezo yake yeye ambayo ni tofauti na maelekezo ya Mungu,
anakutole kusudi la Mungu anaandika maelekezo yake ili uelekee upotevuni,
utasikia najisikia nikaibe kabisa, najisikia niwe mwana mziki, najisikia nivute
bangi, napenda ukahaba, kumbe ndio maelekezo yaliyonakiriwa na shetani ndani ya
moyo wako.
Unakuta mtu alivyokuwa mtoto mdogo, alikuwa anampenda
Mungu, anasema nataka nimtumikie Mungu, niwe mchungaji, niwe mwimbaji, lakini
mtu huyo akishakuwa mtu mzima anakuwa tofauti kabisa “ukiona upo hivyo ujue
umebadilishiwa moyo”.
Unakuta mtu ameokoka anaolewa na mganga wa kienyeji,
mnamuuliza mnamwambia unawaza nini wewe anakwambia Mchungaji nampenda toka
moyoni mwangu, nampenda huyu kaka toka moyoni, ukiangalia kaka mwenyewe ni
mvuta bangi, hata haeleweki. Kumbe moyo wako uliibiwa na shetani na huyo kaka
mvuta bangi akaandikishwa ndani ya moyo wako, bila wewe kujua.
Mtu umeokoka lakini unakuta unampenda binti/kaka wa
kiislamu, kumbe umebadilishiwa moyo, wamenakiri kwenye moyo wako kuwa utaolewa
ana kuoa muislam. Leo tunarudisha mioyo yote uliyobadilishiwa, lazima kusudi la
Bwana litimie, kusudi la Bwana ulilowekewa ndani ya moyo wako tunalirudisha leo
kwa jina la Yesu. “Daudi alisema eeh moyo wangu na vyote vilivyo ndani yangu
mche Bwana”.
Shetani anajua issues zako zote za maisha yako zinatokea
moyoni, kiu yako ya kuimba, kuhudhulia ibadani, kutoa fungu la kumi, kumtumikia
Bwana vyote huanzia moyoni. Shetani ili abadilishe kusudi lako anaiba moyo,
anabadilisha kusudi lililonakiriwa na Mungu moyoni mwako, anaweka maelekezo
yake, unajikuta uliyokuwa unatenda hutendi tena, unaingiwa na kiu ya kutenda
mambo mengine ambayo hujawahi hata kuyawaza. Lakini wewe ukikaa unaona upo
sahihi sababu unachokifanya kinatoka moyoni, kumbe umebadilishiwa moyo ili
uelekee upotevuni.
Kuna watu huwa wanajuta baada ya kutenda jambo,
usiangalie kwamba hili jmbo linatoka moyoni mwangu, cha kufahamu ujue huo moyo
ni wa kwako, unayoyatenda ni kusudi la Bwana tangu awali? Huu ni wakati wa
kukana maelekezo ya moyoni mwako kama sio kusudi la Mungu. Shetani amepanda
jambo ndani ya moyo wako umeanza kulitumikia, kumbe ni kusudi lililopandwa na
shetani.
Shetani akitaka kukuandikia maelekezo yake, huwa lazima
usumbufu utokee, ulikuwa unajiweza vizuri kifedha, ghafla unakosa hela ya kula,
hata hela ya kwenda kanisani huna, kazi unafukuzwa kumbe ni shetani anakuandaa
kukuchomoa kwenye lile kusudi la Mungu, ukishaona umechoka hueleweki shetani
anakuambia hilo sio kusudi lako, anakubadilishia maelekezo yaliyondani mwako
“mara unaalikwa kwenye semina ya “empowerment”, kumbe shetani ndio anakuwa
anakutengeneza kwenye kusudi lake.
Leo ninamlazimisha shetani na watenda kazi wake wote
kurudisha mioyo yenu ya asili irudi kwenu, na moyo wako unarudi kwa jina la
Yesu. Unarudi kwenye kusudi lako la milele.
Namna ya kuomba
Ngo’a maelekezo ya kishetani yaliyopandwa ndani ya moyo
wako ili yakuongoze kwenda mbali na kusudi lako la milele, nayaondoa maelekezo
hayo kwa jina la Yesu. Ninakataa maelekezo yaliyowekwa ndani ya moyo wangu
kugeuza kusudi la Mungu ndani yangu, kama niliandikiwa kuwa muombaji narudisha
kusudi hilo kwangu kwa jina la Yesu, ninakataa kiu ya miziki ya kizazi kipya
ndani yangu, kiu ya uzinzi, kiu zote za kishetani kunipindisha na kusudi langu
la milele nakataa kwa jina la Yesu.
Leo namng’ang’aniza shetani na malaika zake na majini
yake na vibwengo vyake warudishe moyo wako kwa jina la Yesu. Maelekezo ya
kishetani yalioandikishwa ndani ya moyo wangu ili kunipeleka mbali na Mungu
nayakataa kwa Jina la Yesu, maelekezo yaliyonipeleka mbali na baraka zangu naukataa
moyo wenye maelekezo hayo kwa jina la Yesu, anza kudai moyo wako, moyo wa
kumcha Bwana, moyo wa ubunifu, moyo wa mafanikio, moyo wa safari nautaka moyo
wangu kwa jina la Yesu.
Moyo wa kiburi mlioniwekea naukataa kwa jina la Yesu,
moyo wa mauti mlioniwekea naukataa kwa jina la yesu, nautaka moyo wangu kwa
jina la Yesu. Nataka moyo wangu, moyo wa ushindi, moyo wa kushika fedha, moyo
wenye msimamo, moyo unaompenda Yesu, naurudisha moyo wangu katika jina la Yesu
Kristo.
Thursday, November 21, 2013
Jifunze Neno
3:40 AM
No comments
Utangulizi:
Kila mwanadamu katika maisha yake ya hapa Duniani mbali na mwisho wake bado anayo hatima ya maisha yake Mungu aliyomkirimia au kumjali hilo ndilo analolisumbukia kila inapoitwa siku, na wengi hatima zao hizo zimepindishwa na Muovu Bila wao kujuwa au kwa kutojuwa lakini wakakosa msaada katika somo hili ninataka nikurudishe katika ile hatima yako iliyopindishwa katika jina la yesu,
Hatima katika maisha ni nini?
Hatuwezi kujifunza hapa bila kujuwa maana ya kile ninachokiongelea Hatima Ni Hali au uwezo Wa mtu kufikia katika mipango au malengo yake kama alivyoiona au kupanga moyoni mwake, maisha ni ule uwepo wa uhai wa kiumbe chochote amacho kipo katika hii Dunia, sasa uhai wako unaambatana na mahitaji yako ili huu uhai uendelee kuwepo hadi kufikia kusudio la Mungu, kila kiumbe chenye Uhai kina mahitaji yanayo hitajika, hiyo ndioinafaya mipango iwepo ili kufikia ile hatima,
Mithali 16:1 Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana.haya maandaliyo ya moyo ni mipango ya hatima yako kumbuka katika moyo ndiko Roho mtakatifu anapaswa kukaa na ndiko karakana ya kuunda kila unachokitaka kitokee,
Kitabu cha Petro ni waraka wake kwa watu wote; ukisoma, 2 Petro 1:3 “kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe.
Neno la Mungu linamaanisha kuwa uweza wa Mungu umetupatia vitu vyote, kwa kumjua yeye. Kumbe hapa tunapata kujua kuwa ni mapenzi ya Mungu tuwe na vitu vyote, na uweza huo wa Kiungu umeshatupa tayari kila kitu kitupasacho kuishi.
Tunajifuna hapa nini kabla ya maisha yetu kuanza Mungu alikuwa ameshatukirimia mambo yote. Yaani Hatima ya maisha yako Ukisoma Yeremia 1:4 “kisha neno la bwana likanijia Yeremia…” Biblia inapotaja neno inamaanisha “Mungu” kwasababu katika (Yohana 1:1-5) Biblia inathibitisha kuwa neno hilo ni Mungu mwenyewe. Yesu Kristo ndio neno lililokuwa linawajia manabii hapo kabla,
Tunajifuna hapa nini kabla ya maisha yetu kuanza Mungu alikuwa ameshatukirimia mambo yote. Yaani Hatima ya maisha yako Ukisoma Yeremia 1:4 “kisha neno la bwana likanijia Yeremia…” Biblia inapotaja neno inamaanisha “Mungu” kwasababu katika (Yohana 1:1-5) Biblia inathibitisha kuwa neno hilo ni Mungu mwenyewe. Yesu Kristo ndio neno lililokuwa linawajia manabii hapo kabla,
Hivyo kwa kuwa Yesu ndiye Neno tunaweza kusema kwamba Yesu alipomjia Yeremia akamwambia, (Yeremia 1:5) “kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa;” Kumbe Yesu alimjua Yeremia kabla ya kuumbwa tumboni. Kimsingi, Hakuna mtu ambaye anaweza kukumbuka kipindi yupo tumboni wala kabla ya kuwa tumboni,wakati mwingine hata mama mjaamzito kuna wakati siku zinamchenga siku ya yeye kupata Mimba ila Mungu hachengwi kwa jambo lolote,
Mungu alikujua kabla ya kuwepo tumboni na alikukirimia vitu vyote. Swali la kujiuliza wewe mwenyewe hapo ulipo kama Mungu alikujua tangu huko mwanzo, Tumboni mwa Mama yako na alikukirimia kila kitu yaani akakupatia hatima yako yote kwanini maisha yako bado yapo hivyo yalivyo sasa,?
Hapo ndipo Utakubaliana na Mimi ya kwamba Hatima yako imepindishwa,Japo si rahisi kulifahamu hili ila maandiko matakatifu ya tatusaidia kujuwa Hatima yetu imepindishwa wapi,imepindishwa vipi na nani? Tuangalie maandiko
Muhubiri 10:7 Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi, na wakuu wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa.
Kumbe hatima ya mtu kupindishwa haijalishi wewe unacheo gani ua umesoma kiasi gani hapa wakuu wanaostahili wanatembea na miguu watumwa wanafurahia juu ya farasi, ndivyo maisha unayoyaishi maisha yako unayostahili hauyaishi wanaishi watu wengine wasiyostahili na wewe unaendelea kutaabika,
Tukirudi kwa habari ya Yeremia, Mungu aliongea na Yeremia akiwa kijana mdogo kuwa yeye amewekwa kuwa nabii wa mataifa (Yeremia 1:5).
Kumbe kabla hujazaliwa Mungu alikwishakuweka katika njia ya Hatima ya maisha yako kama Yeremia; Jiulize nini kimetokea hadi leo upo kwenye njia nyingine? Mungu alikuwekea mafanikio tangu mwanzo, lakini jiulize nini kimetokea hadi leo upo katika hali hiyo isiyoeleweka hata na wewe mwenyewe?
Kuna watu maisha yanawachanganya hadi wao wenyewe wanashindwa kujielewa kwanini wapo hapa Duniani, hii inawapelekea hata wengine kukatatamaa,
Yawezekana wewe ni maskini leo, lakini unatakiwa ujue pia Mungu hakuiti kwa jina la umaskini bali anakuita kwa jina ambalo ndilo Hatima yako.
Yawezekana wewe ni maskini leo, lakini unatakiwa ujue pia Mungu hakuiti kwa jina la umaskini bali anakuita kwa jina ambalo ndilo Hatima yako.
Japo inanisikitisha sana kwa Yule mtu anayesema kuwa eti! amekubali Matokeo ya yeye kuishi katika maisha anayoyaishi, si mpango wa Mungu wewe utaabike na wala Yesu hakuwa masikini kama vile watu wengine walivyo karirishwa kama yesu alikuwa masikini uwezo wakulisha watu Maalfu kwa maalfu aliutoa wapi ni masikini Gani mwenye uwezo huo,
Warumi 8:29-30 “maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.
Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita na wale aliowaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki, hao akawatukuza” kumbe tunaona kuwa Mungu amekwisha kuchagua tangu asili na tangu asili Hatima yako inaongelewa naMungu.
Na ukisoma mipango ya Mungu juu yako, hutaona kuwa unatakiwa kuishi hivyo unavyoishi kwa kuharibu mimba, au matatizo ya ndoa, au mateso ya umaskini, au kutokufanikiwa au magonjwa ambayo yanayokusumbua sasa. Kukataliwa katika jamii Yeremia 29:11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.
Hivyo mwanzo mwisho Mungu anakujuwa na kukujali na Hatima ya maisha yako iko pale pale Inawezekana ulitakiwa kuwa Mbali sana ki-Roho na kimwili ila hatima yako imepindishwa na yule muovu, kwamaslahi yake
Kuna mambo makuu na makubwa ambayo Mungu anakuwazia katika maisha yako lakini hayajakamilika kwasababu njia uliyotakiwa kupita imekwepeshwa
(Waefeso 3:20 Malaika alipomtokea Gideoni alimwita kwa jina la “shujaa”. Japokuwa Gideoni alikuwa mtu wa kawaida kwa wakati ule bado kumbe tangu tumboni aliitwa shujaa na alitakiwa kuwa shujaa. Tatizo ni maisha yaliyomzunguka yalimfanya asiujue ukweli huu kuwa yeye ni shujaa. Hata wewe maisha yaliyokuzunguka yanakufanya usijitambuwe kuwa hatima yako ni ipi na wewe ni nani kilingana na Hatima yako,
Pamoja na yote jina lile halikubadilika mbele za Mungu kuwa yeye katika ulimwengu wa roho anaitwa shujaa. Je wajua kuwa kabla ya kuzaliwa ulikuwa kwenye mapafu ya Mungu yaani ulikuwa pumzi ya Mungu, ulikuwa pamoja na Mungu ndio maana biblia inakuita “mwana wa miungu” (Zaburi 82:6),
hiyo ndio asili yako. Rudi kwenye asili yako leo, asili yako sio uzinzi na uasherati, sio madeni, sio magonjwa, sio kushindwa. Amua kurudi kwenye asili yako kwasababu tupo duniani Kwa kusudi la Mungu “mpango” huwezi kufa ukiwa kwenye njia ya Mungu mpakamipango yako ikamilike, wakunyweshe sumu wakuloge hutokufa mpaka ukamilishe Hatima yako.
Kuna watu, kwasababu ya maisha wanayopitia wamejikuta wakijiuliza kuwa Mungu yupo kweli? Unawaza kama Mungu angekuwepo usingepitia kwenye mateso yako? Ni muhimu kujua Mungu alishakukirimia vitu vyote tatizo ni kwamba watu wengi hawapo katika asili yao.na hatima yao ilisha pindwa
Kuna watu, kwasababu ya maisha wanayopitia wamejikuta wakijiuliza kuwa Mungu yupo kweli? Unawaza kama Mungu angekuwepo usingepitia kwenye mateso yako? Ni muhimu kujua Mungu alishakukirimia vitu vyote tatizo ni kwamba watu wengi hawapo katika asili yao.na hatima yao ilisha pindwa
Biblia inasema Mungu ametukirimia vyote kwa kumjua yeye, sasa unachotakiwa kufanya ni kurudi katika njia, kwa kuanza
· kusoma neno,
· kufanya maombi yaani unatakiwa ubadilishe staili yako ya maombi na uhamie kwenye maombi ya kushindana ili kurudisha asili ya maisha yako.
Waefeso 6:12 Omba Kwa kushindana Na falume yaani serekali ya Nguvu za Giza,
Kuna mashetani na wachawi ambao wapo katika ulimwengu wa roho ili kubadili Hatima yako ambayo Mungu alikuwekea ili uiishi. Inawezekana Mungu alikuweka kuwa kiongozi mkubwa na mwenye kukubalika
lakini wachawi na mashetani waweza kukuhamisha kutoka katika njia ya Mungu aliyokuitia. Amua kurudi katika Hatima yako ambayo Mungu alikuita kwayo.
Warumi 8:19-21 Yaani hata viumbe vinavyoishi duniani vimetiishwa chini ya uharibifu yaani vimehamishwa kutoka katika asili yao. Viumbe navyo vyajua kuwa havipo katika asili yake, ndio maana navyo vinatarajia kufunuliwa kwake Kristo Yesu ili virudi katika asili yao.
Warumi 8:19-21 Yaani hata viumbe vinavyoishi duniani vimetiishwa chini ya uharibifu yaani vimehamishwa kutoka katika asili yao. Viumbe navyo vyajua kuwa havipo katika asili yake, ndio maana navyo vinatarajia kufunuliwa kwake Kristo Yesu ili virudi katika asili yao.
Hata Hana aliposumbuka miaka mingi pasipo kupata mtoto alimwomba BWANA akasema ukinipa mtoto atakuwa mjakazi wako, hapo ndipo Mungu alipomuingiza nabii Samweli kwenye tumbo la Hana. (1Samweli 1:11) Nabii Samweli ni nabii aliyekuwa na nguvu za Mungu, ambaye Mungu alimtumia sana; kumbe asili yake ni ile iliyotajwa na Hana akiwa kwenye maombi kabla hata ya Samweli kuzaliwa. Amini usiamini maisha unayoishi, sio ambayo Mungu alikupangia wewe uishi; hata wewe mwenyewe ni shahidi kuwa maisha hayo siyo uliyotaka kuishi.
Kuna mashetani wamepindisha asili yako na kukupa maisha mengine na bahati mbaya zaidi umekubali maneno ya watu kukwambia “vumilia vumilia”. Kuna muda unatakiwa uamue kuchukua hatua ya kupambana ili urudi kwenye asili yako.
Ndio maana watu ambao hawachukui hatua ya kuomba maombi ya Kupambana wanajikuta wanahama kila kanisa bila mafanikio kumbe unatakiwa ufanye maamuzi ya kushindana na falme za giza. Huu ni wakati wa kuamua kurudi kwenye asili yako uliyopangiwa na Mungu.
Sikuzote shetani hufanya vita na watu ambao tangu asili waliitiwa maisha mazuri, yeye (shetani) huwahamisha na kuwafanya wawaze kuwa wanavyoishi sivyo Mungu anavyowataka waishi.
Sikuzote shetani hufanya vita na watu ambao tangu asili waliitiwa maisha mazuri, yeye (shetani) huwahamisha na kuwafanya wawaze kuwa wanavyoishi sivyo Mungu anavyowataka waishi.
Leo amua kurudi katika asili yako, pambana na mamlaka za giza. Imeandikwa kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama bali ni juu ya falme na mamlaka za giza. Kataa kuishi maisha hayo na uamue kurudi kwenye asili yako aliyokupangia Mungu. Mungu hakukupangia mateso hayo unayopitia,
Popote ulipo kama Umeshiriki somo hili niwakati wako mzuri wa kuanza kuomba maombi ya kupambana kama maandiko yanavyo sema
Kubukumbu 1:7 Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;
Na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako.
Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani.
Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako.
Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo. Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. Fanya maombi Yakurudishwa katika hatima yako
Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani.
Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako.
Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo. Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. Fanya maombi Yakurudishwa katika hatima yako
Waefeso 6:12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Mungu akubariki sana wewe kushiriki somo hili pia limefafanuliwa zaidi katika DVD Ukihitaji somo hili linapatikana madukani na pia ikiwa hazijakufikia hapo ulipo piga simu kuagiza utatumiwa na utatazama na kusikiliza chumbani kwako, na utapata nafasi ya kushiriki maombi ya kurudisha hatima piga simu uagize Nakala yako
1. DVD HATIMA ILIYOPINDISHWA
2. DVD UPENYWE WA KUMILIKI
3DVD SIRI KUU 3 ZAKUTUZA SIRI ZAKO ZOTE
0756 809 209/0653 294219/0786608801
Kwa Mtumishi wa Mungu,Samson o Mboya