Mtumishi wa Mungu Samson akiwa amewasili mkoani Morogoro na Bendi ya kanisa la Calvary assemblies of God kutoka Mkoani Geita

Bibi akifanyiwa maombi ya uponyaji wa miguu na Nabii Samson o Mboya

Ibada ya lugha Mbili, kiswahili na kingereza

Mamia ya watu wakihudumia katika ile hema ya kinabii pale mkoani Geita maeneo ya Nyankumbu,karibu n bria ya Polisi ibada iliyoongozwa na Nabii Samson o mboya

Prophet Samson akifundisha juu ya kuishi maisha ndani ya ufalme wa Mungu,

Mtu wa Mungu akitamka Neno la kinabii juu ya maisha ya watu waliyoudhuria

Kutana na Neema ya Kinaii Ndani ya Hema ya Kinabii

Thursday, June 18, 2015

Namna ya kugeuza maisha yako

MGUSO WA NENO LA MUNGU Na Mtu wa Mungu Nabii Samson Mboya Ndani ya Hema ya kinabii Bonde la uzima Nyankumbu Tanzania UTANGULIZI: Ujumbe huu ni ujumbe ambao waweza kubadilisha maisha yako kama utaamua kufungua moyo wako, kwasababu mwenendo wa maisha waweza kukufanya uhisi kuwa hakuna matumaini lakini leo baada ya kufutilia somo hili uwezekano wa Maisha yako kubadilika ni mkubwa sana naamini hivyo katika jina la Yesu sema amina…… Kila Neno la Mungu lina pumzi hai mtaji wako ni kuamini , muone Mtumishi wa Mungu hapa Ezekeli , Ezekieli 37:11 "kisha akaniambia, mwanadamu mifupa hii ni nyumba yote ya Israeli tazama wao husema mifupa yetu imekauka matumaini yetu yametupotea, tumekatiliwa mbali kabisa" Ukiendelea kufuatilia kwa karibu kwa habari ya Ezekieli utagundua sababu ya Mungu kumleta katika bonde lile lililojaa mifupa. Kwanza, Imani ya Ezekieli ilikuwa imani yenye matumaini. Ingawa hali halisi ya mifupa ilikuwa imekwisha kauka, yeye alibaki na tumaini kuwa mifupa ile yaweza kuishi. Hatua kubwa sana ya kudhihirisha kuwa mtu anamjua Mungu, ni ile ambayo mtu mmoja katikati ya vita, au hali za kukatisha tamaa, au hana analolitegemea katika maisha yake lakini bado anataja mambo yajayo, anataja matendo makuu ya Mungu anamwamini na kumtumaini Mungu Mungu hapendi ukate tamaa, wala umkufuru yeye katikati ya magumu na kwa taarifa yako tu ni kuwa watu wakubwa katika biblia hata walioitwa na Mungu, walipitia magumu sana lakini katikati ya magumu hayo walitamka maneno ya ushindi. Pia, kutamka maneno ya matumaini katikati ya magumu kunakufanya utoke mapema kwenye hali mtu aliyokoau anayopitia Inawezekana unapitia katika hali ngumu kwa sasa, lakini utakalolinena ukiwa katika dhiki hiyo itakufanya ama utoke ukiwa shujaa au aliyeshindwa. Na ndio maana hata Ezekieli alipowekwa mbele ya mifupa mikavu na kuulizwa 'je mifupa hiyo yaweza kuishi?' Naye alijibu kuwa 'wewe Bwana wajua', akionyesha kuwa hakuna jambo la kumshinda Bwana. Na ndio maana hata alipopewa nafasi ya kutamka neno alitamka uzima. Ni muhimu kujua maneno ya kutamka pindi unapopitia katika hali ngumu. Ni muhimu kujua unachokiongea leo ndicho utakachokiishi kesho na maandiko yanajifunua kwetu tutashiba matunda ya kinywa chetu isijishibishe sumu itakayokumaliza pole pole wengine hujikuta wanaongea maneno mabaya juu yao wenyewe, huku wakisahau kuwa ni shetani ambaye anawafanya waongee maneno hayo ili apate nafasi ya kuharibu maisha yao baadaye. Isaya 57:10 "ulikuwa umechoka kwaajili ya urefu wa njia yako, lakini hukusema hapana matumaini, ulipata kuuhishwa nguvu zako, kwasababu hiyo hukuugua" kumbe watu hawa, hali yao halisi iliwafanya wakate tamaa ya kufika wanapokwenda lakini pamoja na urefu wa njia bado walikiri kuwa matumaini yapo. Na kwasababu ya ukiri huo walipewa nguvu mpya. Usikiri udhaifu, Mungu anayetenda miujiza yupo na ukimkimbilia yeye, ataiondoa aibu yako na kukuvika kicheko. Ukifuatilia habari ya Yusufu ambaye maisha yake yalianza kwa kuuzwa na ndugu zake kwa wamisri. Na alipouzwa waliigawa kanzu yake maana yake aliuzwa bila mavazi, lakini akiwa Misri na matumaini yakaanza kuja likatokea jambo jingine la kukatisha tamaa. Mke wa potifa akamsingizia kuwa anataka kumbaka, hivyo akatupwa gerezani maisha katiaka hali hiyo ni dhahiri kuwa Yusufu alikata tamaa kabisa. Lakini alipotoka gerezani Yusufu akawa waziri mkuu, jiulize, Mungu aliyemfanya kuwa waziri mkuu alikuwa wapi kipindi anauzwa? Au jiulize alikuwa wapi kipindi anawekwa gerezani? Anasingiziwa kubakwa Ruhusu kusudi la Mungu lifanyike katika maisha yako Ni muhimu kujua kuwa sio kuwa kwa unayopitia hali ngumu ukahisi Mungu amekuacha, si kweli; Mungu bado yupo pamoja na wewe na matumaini bado yapo. Yesu Kristo ni tumaini la kutosha kwenye maisha yako. Leo sikia sauti yake hii ikisema. Pata muda kuingia kwenye maombi na Mungu anakupa tumaini jipya leo. Inawezekana unapitia shida za ndoa, matatizo kazini, vita shuleni, huduma ni ngumu watumishi wengine wamekuinukia roho ya kukataliwa mpaka umejihisi hakuna kesho ile uliyoiwaza jana Leo tambua kuwa hata Ayubu katikati ya dhiki kuu hakuwahi kumkufuru Mungu Niko ambaye niko jina lake bali aliweka tumaini lake kwake na kwa saa sahihi matumaini makuu yalionekana.Tunajifunza kwao maana walishinda swali ushindi wako uko wapi? Ili wengine wapate shule ya kujifunza? Hata kama ndoto yako inaonekana inataka kuzimika, inawezekana ulikuwa na ndoto za kusoma katika maisha yako lakini sasa unaona muda umeenda nakwambia bado lipo tumaini. Inawezekana madktari walikwambia kuwa mwisho wa kuzaa ni miaka 45 na wewe sasa unajiona unaelekea huo umri ukiwa hauna mtoto;unmechumbiwa na wanaume wengi hakuna anayekamilisha Harusi kiasi sasa unahisi aibu kwa jamii, umechelewa kuowa unahisi kuwa uko na mikosi usiogope Mungu bado yopo kwaajili yako na anakupenda kuliko mwanadamu yeyote youle uliyewahi kumfahamu lakini nakwambia neno ambalo Yesu amenituma kwalo kuwa USIKATE TAMAA

Unamguso katika jamii?

KUWA CHUMVI Na Mtu wa Mungu Nabii Samson Mboya UTANGLIZI: Ninamshukuru Mungu kupitia Yesu kristo kutupatia wakati huu mzuri mimi na wewe tujifunze kupitia mfano wa chuvi, bilashaka Mfano huu ulitumika ili kuwa rahisi kila mtu kuelewa kirahisi kwakuwa chuvi inatumika sana katika chakula, kama kiungo japo hakina sifa kubwa ila kina umwihimu mkubwa, katika chakula, watu wengi wanampenda Mungu ila kuishi maisha Mungu anataka ni ngumu kwao swali la mwisho katoka somo hili, chumvi ikipoteza ladha yake itakolezwa na nini? Mafundisho mengi yamegeuzwa na ibilisi badala ya watu kuwa chuvi wana tafta viyu na kutumia ili vilete ladha ya chuvi mafundisho yanakuwa yanalenga utajiri tu Kuelekeza watu kwa Kristo kwa ajili ya kupata utajiri ni udanganyifu na pia ni hatari. kwa sababu Yesu alipotuita, alinena mambo kama: “Vivyo hivyo, basi, hakuna hata mmoja wenu atakayekuwa mwanafunzi wangu kama asipoachilia kila kitu alicho nacho” (Luka 14:33). Hatari kwa sababu kutambulisha utajiri au mali badala ya kristo ni kujiingiza kwenye uharibifu ”Kimwili na ki-Roho na ladha ya mali haidumu, (Timotheo 6:9). Kwa hivyo huu ni ombi langu kwa wale wanaohubiri utajiri. . kuwa na ladha ya mali badala ya chumvi ni kubadilishia watu ladha Yesu alisema, "Jinsi gani itakavyokuwa vigumu kwa matajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu!" Wafuasi wake walishangazwa, kama vile wengi waliomo katika chama cha “utajiri” wangeshangazwa. Naye yesu akaendelea kuwashangaza zaidi akisema, “Ni rahisi zaidi ngamia kupenya katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu." Wakajibu kwa kutoamini: "Ni nani basi, atakayeweza kuokoka?" Yesu akawaambia, "Kwa binadamu haiwezekani, lakini kwa Mungu si hivyo, maana kwa Mungu mambo yote huwezekana"(Mariko 10:23 -27). Swali langu kwa wahuibiri wa utajiri ni: Kwa nini unataka kujenga huduma ambaye inaifanya kuwa ngumu kwa watu kuingia mbinguni? Usijenge huduma ambaye inaleta maafa kwa watu. Paulo alisema, “Kweli dini humfanya mtu awe tajiri sana, ikiwa anatosheka na vitu alivyo navyo. Maana hatukuleta kitu chochote hapa duniani, wala hatutachukua chochote. Kwa hiyo basi, kama tunacho chakula na mavazi, tunapaswa kuridhika navyo.” Lakini alikanya majaribio ya kutaka utajiri. Vile vile, alikanya kuhusu wahubiri ambao wanaubiri kuhusu utajiri badala ya kusaidia watu kulikwepa. Alisema, Lakini wale wanaotaka kutajirika huanguka katika majaribu, na kunaswa katika mtego wa tamaa nyingi mbaya za kipumbavu, ambazo huwavuta mpaka kwenye uharibifu na maangamizi. Kwa maana kupenda sana fedha ni chanzo cha uovu wote. Watu wengine wametamani sana kupata fedha hata wakatangatanga mbali na imani, na wameivunja mioyo yao kwa huzuni nyingi” (1 Timotheo 6:6-10). Kwa hivyo swali langu kwa wahubiri wa utajiri ni: Kwa nini mnataka kujenga huduma ambaye inaelekeza watu kudunga mioyo yao kwa huzuni nyingi na kuwavuta kwenye maharibifu na uhangamizi? Usijenge huduma ambaye inaendeleza uwezekano wa kuharibiwa kwa nondo na kutu. Yesu alionya katika juhudi za kujiwekea hazina hapa duniani. Anatuhimiza kuwa tusijilimbikizie mali zinazoharibu, na wezi huingia na kuiba. Jiwekeeni hazina mbinguni ambako nondo na kutu hawawezi kuiharibu, wala wezi hawaingii wakaiba” (Mathayo 6:10). Paulo alisema hatufai kuiba. Maana yake ilikuwa kufanya kazi kwa bidii tukiwa tukitumia mikono yetu. Lakini sababu hasa haikuwa kujiwekea au kuhifadhi. Sababu ilikuwa “kuweza kupeana.” “Aliyekuwa akiiba, asiibe tena, bali na aanze kufanya kazi njema kwa mikono yake, apate kuwa na kitu cha kumsaidia mtu aliye maskini.” (Efeso 4:28). Hili sio changamoto kwa wale wanaotaka kutajirika kwa ajili ya kuweza kupeana zaidi. Hakuna sababu ambaye inamfanya Yule anayetengeneza 100000 kuishi tofauti na Yule ambaye anayetengeneza 10000. Tumia fedha vizuri;. Sababu gani unachochea watu kufikiri kwamba wanahitaji kuwa na mali ndiposasa waweze kupeana? Kwa nini usiwahimize kufanyisha maisha yao yawe ya kawaida na waweze kutoa hata zaidi? Ingekuwaje kutoa kwao kuwa shuhuda kubwa kwamba Kristo, na sio rasilmali, ndio hazina yao? Sababu ya mwandishi wa Ebrania kutuanduikia kutosheka na tuliyo nayo ni kwamba kinyume chake inamaanisha imani ndogo katika ahadi za Mungu. Asema, “Msiwe watu wa kupenda fedha; toshekeni na vile vitu mlivyo navyo. Mungu mwenyewe amesema: ‘Sitakuacha kamwe, wala sitakutupa.’ Ndiyo maana tunathubutu kusema: ‘Bwana ndiye msaada wangu, sitaogopa. Binadamu atanifanya nini?’” (Ebrania 13:5-6). Ikiwa Biblia inatuhimiza ya kuwa kutosheka na tulionayo inaheshimu ahadi ya Mungu kutotupa sisi, ni sababu gani tunafundisha watu kutaka kutajirika? Usijenge huduma ambayo inachangia kwa watu wako kunyongwa hadi kufa. Yesu anakanya kwamba neno la Mungu, ambaye inafaa kuleta uhai, inaweza kunyongwa na kutolewa uwezo wake na utajiri. Asema ni kama mbegu ambaye inamea kati ya miiba yatakayoinyonga hadi kifo: “Zile zilizoanguka kwenye miti ya miiba ni watu wale wanaosikia lile neno, lakini muda si muda, wanapokwenda zao, husongwa na wasiwasi, mali na anasa za maisha, na hawazai matunda yakakomaa” (Luka 8:14). Usijenge huduma ambao unautoa utamu katika chumvi na kuficha mwangaza kikapuni. Ni nini hufanya wakristo kuwa chumvi ya dunia na mwanga wa ulimwengu? Hakika sio mali. Mapenzi ya utajiri na ufuataji wake inaonja na pia inafanana na ulimwengu. Haipatii dunia chochote tofauti na yale ambaye imekwisha amini. Pigo kubwa kwa mahubiri ya utajiri ni kwamba mtu hapaswi kuwa ameamshwa kiroho ndio aweze kuipokea; mtu anahitaji tu kuwa mchoyo. Kutajirika katika jina la Yesu si chumvi ya dunia au mwanga wa ulimwengu. Katika hayo, dunia huona tu picha yake. Na ikiwa ina maana, wataipokea. Yesu, aliponena, hutuonyesha ni nini maana ya chumvi na mwanga. Ni kutaka kwa furaha kuteseka kwa ajili ya Kristo. Yesu alisema, "Heri yenu ninyi watu wakiwatukana, wakiwadhulumu na kuwasingizia kila aina ya uovu kwa ajili yangu. Furahini na kushangilia maana tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Hivyo ndivyo walivyowadhulumu manabii waliokuwako kabla yenu. Ninyi ni chumvi ya dunia! Lakini chumvi ikipoteza ladha yake itakolezwa na nini? Haifai kitu tena, ila hutupwa nje na kukanyagwa na watu. Ninyi ni mwanga wa ulimwengu! Mji uliojengwa juu ya mlima hauwezi kufichika” (Mathayo 5:11-14). Kitakachofanya dunia ionje (chumvi) na ione (mwanga) wa Kristo ndani yetu si ya kwamba tunapenda utajiri jinsi wanavyoipenda. Bali, itakuwa matayarisho na uwezo wa wakristo kupenda wengine kupitia mateso, ilhali wakisherekea kwa sababu malipo yao imo na Yesu mbinguni. Kwa kawaida, mambo haya ni magumu kwa binadamu. Ni mambo ya kiroho. Lakini kuvuta watu na ahadi ya utajiri ni jambo la kawaida na sio ujumbe wa Yesu. Yesu hakufa iliwa watu wapate utajiri wa ulimwengu huu. Mawasiliano zaidi kwaajili ya ushahuri na maombezi piga simu 0756 809 209

Friday, February 14, 2014

Habari njema kwa Mkoa mpya wa geita

Yule mtu wa Mungu  Nabii Samson sasa ile hudumuma ya Ushahuri na Maombi anatoa pia na kwa njia ya Simu namba 0756 809 209

Tuesday, January 14, 2014

Mungu anataka uwe vile anataka yeye siyo vile unataka wewe,

Mungu amempa mtumishi wake Nabii Samson Neema ya kutafsiri  picha na njozi  hii ni Neema ya ajabu kwa Msaada fika pale katika Hema ya Kinabii au Piga simu 0756 809209

Wana wa Manabii ndani ya Hema ya kinabii

Furaha ya tawala Ghafla kabla Mtu wa Mungu kuanza kutoa Neno la kinabii,

Thursday, December 12, 2013

Kutana na Mama Nabii katika Maombii maalumu ya kuteka kabla ya kiingia Mwaka mpya Ndani ya Hema ya kinabii

Ni ule usiku wa mwaka mpya utakaoambatana na maombii Maalumu yatakayoonozwa na Mke wa Nabii Samson,

Baada ya miuujiza mikubwa kutendeka ndani ya Hema ya kinabii, wananchi kwa furaha kubwa wakishangilia na matawi kutoka kila kona. ya kinabii

Hatimaye nyankumbu mkoni Geita yageuka kuwa kisima cha baraka ,baada ya wanakijiji wa nyankumbu kushangazwa na matendo makuu ya Mungu pale mabubu wawili walipoongea!Jambo hili lilitokea baada ya maombezi ya mtu wa Mungu nabii Samson.